MANJI ATETEWA
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/1/27/2016 3:02:11 PM
Tawi la
Yanga Kibaha kwa Mfipa limepinga kauli iliyotolewa na mwenyekiti wa matawi ya
Yanga Tanzania MOHAMED MSUMI kuhusiana na kumpa amri Mwenyekiti wa Yanga,
YUSSUPH MANJI kufuatia hatua ya
kumuachisha kazi katibu wa klabu hiyo.
Mwenyekiti
wa Tawi la Yanga Kibaha kwa Mfipa, MRISHO KHALFAN SWAGALA amesema kuwa
Mwenyekiti wa Yanga YUSUPH MANJI yupo sawa kuhusiana na hatua hiyo na kumtaka
mwenyekiti huyo matawi ya Yanga kumuomba radhi Mwenyekiti Manji ili kuleta
mshikamano klabuni.
SWAGALA
amebainisha kuwa katiba ya Klabu ya Yanga inatambua mamlaka aliyo nayo
Mwenyekiti Manji na MSUMI akiwa kama mwenyekiti wa matawi ya Yanga Tanzania
atambue kuwa yeye yupo chini ya Mwenyekiti Manji na anayo mamlaka kamili ya
kutoa uamuzi kuhusiana na klabu yake.
END.
Comments
Post a Comment