VIDEO-BABU MLEZI AZAA NA YATIMA ANAOWALEA
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/11/5/2015 7:47:04 PM
Katika hali
isiyo ya kawaida suala la kutunza watoto yatima katika jamii limeingia mdudu
kufuatia mmoja ya wanajamii ambao wanajinasibu kulea watoto yatima baadhi yao
wametumia nafasi hiyo kukidhi mahitaji yao ya kimwili.
Hali hiyo
imedhihirika hivi karibuni kufuatia mlezi wa watoto yatima, BW.JOSEPH BAGULE
kuamua kuanza kutembea na watoto anaowatunza na kuzaa nao, hali ambayo
imesababisha wanajamii kustusha wakazi na wanajamii wa mtaa wa Pangani
halmashauri ya mji wa Kibaha na kuamua kuchukua hatua.
Mjumbe wa
serikali ya mtaa BW.EMMANUEL SWAI akizungumza na mwandishi wa Habari hizi,
amebainisha kuwa kwa muda mrefu wao kama wakazi wa mtaa wa Pangani wamekuwa
wanashangazwa na huruma ambayo mzee BAGULE amabyo amekuwa akionyesha kwa watoto
yatima ilihali akiwa anakiuka taratibu zxa kuwalea watoto hao na kuamua
kuwafanya baadhi yao wake zake.
Kwa mujibu
wa wakazi wa mtaa huo, Mzee Josaeph Bagule amekuwa akiwatumia watoto ambao
anadai ni yatima kwa manufaa binafsi na kuwatumia kama vyombo vya
kujistarehesha na kutoa agizo ambalo lina lengo la kupotosha jamii kwamba
anaoishi nao ni watoto wake ikiwa pamoja na mkewe.
Na katika
suala la kushangaza zaidi Mzee huyo amefikia hatua ya kuzuia familia yake
kupata tiba ya kitaalamu jamii ambayo ipo chini yake na hivyo kusababisha vifo
kwa watoto ambao wanapata matatizo ya kawaida kupata huduma ya afya kutokana na
imani yao, ambayo inahusisha kusali ibada ambayo inahusu watu ambao wapo chini
ya him aya yake kutoendfa hospitali kupata tiba mpaka wanapofariki dunia na
kuzikwa maziko ambayo hayafuati mila na desturi za kiafrika na dini.
Mwandishi wa
Habari hiz ameshuhudia makaburi ambayo maiti mbalimbali ambazo zimezikwa kwa
kuzingatia utaratibu wa ajabu ambao unaamini kuwa mtu akishakufa unabaki mzoga
ambao hauna thamani na kufikiwa kama mbwa bila alama yoyote.
BW.JOSEPH
BAGULE akijitetea ameeleza kuwa yeye kama mlezi wa familia hiyo amekuwa
anakabiliwa na changamoto mbalimbali kutoka kwa jamii kuhusiana na kutowapeleka
shule watoto ambao amekuwa anawalea, kutokana nay eye kutokuwa na uwezo wa
kuwasomesha.
Na amekana
kuwatumia watoto hao kama chombo cha kujistarehesha, na kudai hayo ni majungu
ambayo wanajamii wameamua kumvalisha ili kumpaka matope kutokana nay eye
kujiangalia mwenyewe na familia yake.
Kutokana na
kadhia hiyo Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani liliamua kuingilia kati
kulishughulikia suala hilo hili kulipatia ufumbuzi na kuepesha uvunjifu wa
amani ambao ungeweza kujitokeza kutoka kwa jamii amabyo tayari imechoshwa na hali
ambayo wameishudia na hivyo kumtria nguvuni kwa ajili ya maelezo zaidi.
END.
Comments
Post a Comment