Posts
Showing posts from March, 2017
KIBAFA YAFANYA UCHAGUZI
- Get link
- X
- Other Apps
By
BERNARD KOMBA
-
Ben Komba/Pwani-Tanzania/06/03/2017 11:56:39 Chama cha soka wilaya ya Kibaha hatimaye kimepata viongozi watakaokiongoza chama hicho kwa kipindi kijacho, kufuatia kukosa uongozi kwa takriban miaka minane. Katika uchaguzi huo wa KIBAFA, wamefanikiwa kupata Katibu mpya ambaye ni DAUD MHINA na Mwenyekiti wake ni ROBERT MUNISI kwa kushirikiana na viongozi wengine ambao wamechaguliwa katika kuhakikisha wanaendeleza mpira wa soka Kibaha. Akiongea baada ya uchaguzi huo, Mwenyekiti mpya ROBERT MUNISI amewahakikishia wapiga kura kwa pamoja watahakikisha chama hicho cha wilaya ya Kibaha kinakuwa mfano kwa vyama vingine vya wilaya. Akiongea katika uchaguzi huo, Katibu wa Chama cha soka mkoa wa Pwani, HASSAN HASSANOL amekitaka KIBAFA kusimamia maendeleo ya mchezo wa soka wilayani Kibaha ili kuwezesha vilabu vya wilayani hapa kufanya vizuri kwenye mashindano mbalimbali ya soka. Ikiwa na kuzisaidia timu zinazoshiriki ligi mbalimbali nchini katika kukabiliana na changamoto zinazo...
WAKAZI MATIPWILI BAGAMOYO WAPINGA UBABE WA MKUU WA WILAYA
- Get link
- X
- Other Apps
By
BERNARD KOMBA
-
MGOGORO WAIBUKA KUFUATIA UBABE WA DC-BAGAMOYO: Ben Komba/Pwani-Tanzania/28/02/2017 13:12:36 Sakata la uwekaji wa kutumia nguvu wa mpaka kati ya kijiji cha Matipwili na hifadhi ya Mbuga ya Saadani wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani, limeingia katika sura mpya kufuatia Mwenyekiti wa kijiji hicho kubainisha matumizi makubwa ya nguvu katika utekelezaji wa suala hilo kunakofanywa na Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo ALHAJI MAJID MWANGA. Mwenyekiti wa kijiji hicho cha Matipwili, BW. GESANDE MWISA amesema amekuwa akipokea vitisho mbalimbali ikiwa pamoja na majaribio kadhaa ya kutaka kuchonganishwa na wananchi kutokana na msimamo wake kuhusiana na utekelezaji wa mpango huo wa kubadilisha mipaka ambao utaathiri zaidi kijiji hicho. BW. MWISA amesema kuwa eneo la mgogoro halitakiwi kuguswa na pande zote mbili mpaka kutakapopatikana muafaka ambao utawezesha kutoa ufumbuzi wa mgogoro husika. Amesema yeye ananshangazwa na Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo kuamua kufanya jambo hilo kwa nguvu badala ya kus...