HALMASHAURI YA WILAYA YA KIBAHA NA RIPOTI YA UKAGUZI
Ben Komba/Pwani-Tanzania/2012-05-24/17:33:26 Halmashauri ya wilaya ya Kibaha ya Kibaha kupitia kikao maalum cha Baraza la madiwani, imesoma taarifa ya ukaguzi wa mahesabu ya kipindi cha mwaka wa fedha 2010/2011 ambayo imebainisha maendeleo ya miradi mbalimbali yenye lengo la kusaidia jamii katika huduma muhimu kama za maji, ujenzi wa miundombinu na utawala. Akisoma taarifa hiyo Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kibaha anayeondoka, BI. AZIMINA MBILINYI, ambaye anakwenda kuwa mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero amesema katika kipindi chake kuna kiasi cha shilingi milioni 32,890,673/=, ambapo zimenuwiwa kuelekezwa kwenye mradi wa ujenzi wa stendi ya mabasi Mlandizi, Na tayari maelekezo yameshatolewa kutengenezwa kwa mpango kazi ambao ambao utatoa mchanganuo wa matumizi ya fedha ambazo zinakadiriwa kufikia shilingi Milioni 30 zitatumbukizwa katika utekelezaji wa mradi huo,m ikiwa na pamoja na shilingi milkiuoni 2,890,00/= kwa ajili ya usimamizi wa mradi huo, na ma...