USHIRIKIANO WA WANANCHI UNAHITAJIKA KUPAMBANA NA UHALIFU
Ben Komba/Pwani-Tanzania/30/08/2016 13:10:17 Kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Pwani imefanya kikao na kamati ya amani ya viongozi wa dini kutathmini hali ya kukosekana kwa amani kunakosababishwa na majambazi ambao wamejichimbia katika wilaya za Mkuranga na Rufiji. Mkuu wa mkoa wa Pwani, MHANDISI EVARIST NDIKILO amesema kuwa mapambano yanaendelea mpaka sasa katika kuhakikisha wanafuta kabisa mtandao huo wa ujambazi ambao umekuwa kitisho kikubwa kwa amani na usalama wa wananchi. BW.NDIKILO amesema kuwa ni juu ya jamii kutoa ushirikiano kwa vyombo vya usalama katika kusaidiana kwenye udhibiti wa vitendo vya uhalifu na hasa ikizingatiwa wanaofanya hivyo ni ndugu zetu au majirani zetu. Ametoa mfano wa kijana Fundi seremala ambaye alimuua Mwenyekiti wa kijiji cha PANZUA ambaye aliishi katika kijiji hicho kwa takriban miaka 25, lakini kwa mshangao wa wengi alichukua hatua ya kumuua mwenyekiti wa kijiji. Aidha ametumia fursa hiyo kutoa onyo kuhusiana na maandamano y...